Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) na moja ya Ligi Daraja la Kwanza (VPL).
Mechi namba 143 kati ya Tanzania
Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8 mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku
moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile Machi 8 mwaka huu Mbeya City itautumia
uwanja huo kwa mechi nyingine ya VPL.
Nayo Mgambo Shooting iliyokuwa icheze
na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa
imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka huu kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa na mechi
mbili.
Kwa upande wa FDL, mechi ya Mkamba
Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka
huu mjini Ifakara. Mechi hiyo imerudishwa nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo
SC kwani Machi 1 mwaka huu itacheza na Burkina Faso mjini Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment