![]() |
| MARSH AKIZUNGUMZA NA ABDUL MOHAMMED WA BBC |
Hali ya
Kocha Msaidizi wa timu ya taifa (Taifa
Stars), Sylvestre Marsh, inaendelea vizuri baada ya kuchukuliwa vipimo kwa mara
ya pili juzi Jumatatu ambapo majibu ya vipimo hivyo bado hayajulikani lini
yatakuwa tayari.
Kocha huyo
ameanza kuugua hivi karibuni ikiwa ni
wiki ya pili sasa tangu alazwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amekuwa akifanyiwa
uchuguzi ili kubaini tatizo linalomsumbua.
Akizungumza
na Championi Jumatano, kocha huyo alisema kwa sasa anaendelea vizuri, japokuwa
bado anaendelea na vipimo.
Marsh alisema
kwa kiasi fulani anaendelea vizuri, japo baada majibu ya vipimo kutoka ndipo
ataanza kupata matibabu zaidi kufuatia madaktari kugundua tatizo lake.
“Nimepata
vipimo siku ya leo lakini sijajua majibu yatatoka lini, hii ni kutokana na aina
ya vipimo nilivyofanyiwa huwa inachukua muda mrefu majibu kutoka, kwa hiyo
nitaendelea kuwa hapa hospitalini mpaka pale nitakapopata majibu.
“Lakini kwa majibu ambayo siyo rasmi, inasemekana kuwa huenda nikawa na uvimbe
katika sehemu ya kifua ambayo chakula hupita, japo siyo majibu ya vipimo
niliyopewa. Majibu yakiwa tayari nadhani ndiyo tutajua ni tatizo gani.
“Zaidi sana
nawashukuru wale wanaojitoa kuja kunijulia hali hapa hospitalini, Mungu
awatie nguvu na wasichoke. Ninaamini
nitapona tu nikiendelea kupata matibabu vizuri,” alisema.
SOURCE: CHAMPIONI








0 COMMENTS:
Post a Comment