Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar iliyochezwa Februari 9 mwaka huu Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 25,602,000.
Watazamaji 8,534 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji Mbeya City kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1. Kiingilio katika mechi hiyo kilikuwa sh. 3,000.
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 3,905,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh.
489,500 wakati kila klabu ilipata sh. 6,256,097.05.
Uwanja sh. 3,181,066.52, gharama za
mechi sh. 1,908,639.91, Bodi ya Ligi sh. 1,908,639.91, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 954,319.96 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya
(MREFA) sh. 742,248.86.







0 COMMENTS:
Post a Comment