Kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’, juzi
Jumamosi alikuwa katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa soka
waliokuwa wakitaka kumkumbatia huku wengine wakitaka japo kumgusa, hali
iliyomfanya apotezane na wachezaji wenzake baada ya mpira kumalizika.
Tukio hilo lilitokea baada ya kumalizika kwa mtanange
wa kukata na shoka kati ya Simba na Mbeya City ambapo matokeo yalikuwa sare ya
kufungana bao 1-1.
Katika tukio hilo, Championi Jumatatu lilishuhudia
umati wa mashabiki hao ukimzingira mchezaji huyo, wengine wakimkumbatia na
kumzuia kwenda kuungana na wenzake mpaka askari wa kutuliza ghasia
walipomsaidia kwa kuwatawanya.
Baada ya mashabiki hao kutawanywa, ndipo Messi ikabidi
aangaze walipoelekea wenzake na kuwafuata.
0 COMMENTS:
Post a Comment