NYOSSO (KUSHOTO) AKIMDHIBITI LUHENDE WA YANGA |
Baada ya kufungwa na Ruvu Shooting bao 1-0, beki wa
Coastal Union, Juma Nyosso, amesema kwa sasa hawaangalii nyuma zaidi wanaendelea kujipanga kwa ajili
ya mchezo ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Februari 22 kwenye Uwanja wa
Mkwakwani, Tanga.
Coastal Union juzi ilipoteza mchezo wake wake wa nne
msimu huu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Beki huyo wa zamani
wa Simba, alisema mchezo ulikuwa mzuri na wenye ushindani, japo wapinzani wao
waliwazidi dakika za mwisho na kufanikiwa kuwafunga kwa bao la dakika ya 85.
Nyosso alisema kwa sasa wanaangalia mbele jinsi gani ya
kupata pointi tatu katika mchezo ujao dhidi ya Mbeya City.
“Kwa sasa tunaangalia ni vipi tunapata pointi tatu kwa
mchezo wetu ujao. Mchezo uliopita umepita, kikubwa ni sisi kupata ushindi kwa
mchezo wetu ujao,” alisema Nyosso.
0 COMMENTS:
Post a Comment