Mwenyekiti wa Klabu
ya Simba, Ismail Aden Rage, ameendelea kumkomalia mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel
Okwi kwa kudai kuwa, suala lake bado lina utata na mtego mkubwa ambao
haujajulikana.
Okwi alikuwa katika
wakati mgumu kufuatia leseni yake ya kucheza ligi kuu kufungiwa na Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), wakisubiria ufafanuzi kutoka Fifa kuhusiana na kesi
zinazomkabili, sasa ameruhusiwa kucheza.
Rage amesema kuwa, suala la Okwi siyo rahisi kama watu
wanavyodhani kwani bado lina utata na kudai kuwa, kuna mtego mkubwa unaomkabili
mchezaji huyo kuhusiana na kesi zake.
“Nani kasema kuwa
Okwi ameruhusiwa kucheza? Mimi nilimsikiliza vizuri Mwesigwa (Selestine –
katibu wa TFF) alivyokuwa akizungumza kuhusiana na suala hilo kwenye vyombo vya
habari.
“Ishu siyo rahisi kama watu wanavyofikiria,
kunatakiwa umakini wa hali ya juu kuhusiana na jambo hilo, kwani alieleza kuwa
kuna baadhi ya mambo hayajakamilika na wanaendelea kufuatilia.
“Kuna mtego mkubwa
sana juu yake watu hawajui tu, inabidi kunapoandikwa habari hii kunatakiwa
umakini wa hali ya juu isije ikawa tofauti, mimi siwezi kutoa ‘komenti’ juu ya
suala hilo kwa sasa hadi hapo litakapopatiwa ufumbuzi lakini nitazidi
kufuatilia fedha za Simba Fifa,” alisema Rage.
0 COMMENTS:
Post a Comment