Hali ya jiji la Mbeya lineonakana kuchangamka
huku kila sehemu ya mji huo gumzo likiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya
wenyeji Mbeya City dhidi ya Simba.
Mashabiki wengi wanaonekana mitaani wakiwa na
jezi za rangi ya zambarau na nyeupe ambayo huvaliwa na Mbeya City na wachache
tu, tena wengi ni wale waliosafiri na timu hiyo kutoka jijini Dar nao wamepiga
uzi mwekundu na weupe.
| MASHABIKI SIMBA WATAKUWEPO KUISHANGILIA TIMU YAO |
Lakini mashabiki wa Mbeya City wanaonekana
kujiamini zaidi kwa kuwa timu yao hiyo haijawahi kufungwa kwenye Uwanja wa
Sokoine tokea ligi inaza na imepoteza mechi moja tu kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar dhidi ya Mabingwa Yanga.
Lakini Simba wamekuwa wakisisitiza leo ni siku ya
kuinyamazisha Mbeya kwa kuwafunga wenyeji wao hao kwa mara ya kwanza tokea
kuanza kwa ligi hiyo, kiti ambacho Kocha Juma Mwambusi wa Mbeya City amesema ni
nadra kutokea.
Katika mechi ya kwanza jijini Dar, timu hizo
zilimaliza mechi kwa sare ya bao 2-2, Mbeya City wakisawazisha mabao yote baada
ya kuwa nyuma kwa mabao mawili. Je, leo itakuwaje? Vuta subira.








0 COMMENTS:
Post a Comment