Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameingia
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati Yanga ikikipiga na timu yake ya
zamani ya Ruvu Shooting na kushangiliwa kwa nguvu na mashabiki.
Mashabiki hao wameripuka kwa furaha baada ya Mkwasa kuingia
uwanjani katika dakika ya 17 wakati mechi hiyo inaendelea.
Mkwasa alikuwa nchini Misri alikokwenda kuisoma Al Ahly
iliyokuwa inacheza dhidi ya CS Sfaxien katika mechi ya Kombe la Super Cup na
kushinda kwa mabao 3-2.
Mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA), Mkwasa alipitiliza moja kwa moja hadi Uwanja wa
Taifa.
Yanga itaivaa Al Ahly katika mechi mechi itakayoigwa
Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment