![]() |
| HUYU MAMA MUUZA MIHOGO YEYE ALIKABIDHIWA TIMU YA WAHARIRI WA CHAMPIONI |
Na Lucy Mgina
IMETIMIA! Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa
kwa hamu na wasomaji wa Gazeti la Championi kujinyakulia shilingi milioni 10
taslimu, sasa imetimia kwani leo kwenye Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar
ndiyo itafanyika droo hiyo ya mwisho.
Hii ni droo ya mwisho ambapo awali
katika droo zilizopita walipatikana washindi mbalimbali wa sofa seti, friji,
flat screen na dekoda yake, dinner seti na nyinginezo kibao.
Meneja wa Global Publishers Ltd ambao ni
wachapishaji wa gazeti hilo, Abdallah Mrisho, alisema ni wakati wa mavuno kwa
wasomaji wake ambao walituma kuponi ili kujishindia kitita hicho.
Alisema kila kitu kipo tayari kwani leo
pia watatoa jezi na zawadi nyingine kibao kutoka kwa Mr Championi kabla ya
mshindi mkubwa kukabidhiwa chake mapema.
Alisema kwa ambao hawajakabidhi kuponi
wazilete mapema leo Jumatatu kadiri wawezavyo kwani hakuna kiwango maalum.
Alizitaja sehemu ambazo unaweza
kuziwahisha kuponi kwa wakazi wa Dar kuwa ni Dar Live Mbagala, Ubungo Terminal,
Magomeni Mwembechai, Mwenge, Kariakoo kwenye ‘round about’, Zahor Matelephone iliyopo Kariakoo, Buguruni,
Ofisi za Global, Mwenge, Tegeta Kona ya Nyuki, Ubungo Yenu Bar na Kigamboni
Feri.
“Ambao bado hawajaleta kuponi zao
wafanye haraka leo asubuhi na mapema wazilete kwani mchana tutakuwa na droo
yenyewe ambayo mshindi atajinyakulia shilingi milioni 10.
“Wasomaji watambue hii ni droo kubwa
ambayo mshindi atapatikana kwa uwazi na itachezeshwa mbele yao, hivyo
hawatakiwi kuwa na hofu,” alisema Mrisho.
Droo hiyo itasimamiwa na ofisa kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board), Emmanuel Ndaki.








0 COMMENTS:
Post a Comment