Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kuwa,
upo tayari kukaa mezani na TP Mazembe kumuuza kiungo mshambuliaji, Ramadhani
Singano ‘Messi’ kwa dau zaidi ya lile alilouzwa mshambuliaji Emmanuel Okwi
katika Klabu ya Etoel du Sahel ya Tunisia.
Simba ilimuuza Okwi kwa dola 300,000
ambazo ni zaidi ya Sh milioni 480 kwenye kikosi cha Etoile du Sahel, lakini
mpaka leo haijapata fedha yoyote kutokana na mauzo hayo.
Hivi karibuni uongozi wa TP Mazembe ya
Lubumbashi, DR Congo ilimtuma kiongozi wa usajili wa timu hiyo ambaye aliangalia
mechi kati ya Simba na Rhino ya Tabora kwa ajili ya kumfuatilia Messi kufuatia kupata
taarifa kuwa yupo fiti.
Ezekiel Kamwaga, alisema iwapo Mazembe itakuwa
inamhitaji mchezaji huyo, wapo tayari kukaa meza moja na kuzungumza ili
biashara ifanyike, kwani hawawezi kumzuia mchezaji yeyote yule iwapo atapata
dili nje na dau lake ni zaidi ya alilouzwa Okwi.
“Kama kuna klabu inamhitaji Messi ije
Simba ili tuweze kuzungumza na tuweze kuangalia maslahi yetu na ya mchezaji
kiujumla.
“Dau la Messi ni tofauti na lile
tulilomuuzia Okwi la dola 300,000. Mauzo ya Messi yatakuwa ya juu zaidi
kulingana na ubora wa mchezaji, pia kwa kuwa anatarajia kuwa katika mpira kwa
muda mrefu zaidi tofauti na ilivyo kwa Okwi,” alisema Kamwaga.







0 COMMENTS:
Post a Comment