Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie
marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya
Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo
vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini
Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa
Kanembwa JKT.
Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF
inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo
wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment