Wakati mechi kati ya Mbeya City dhidi ya
Simba inatarajia kuanza saa 10:30, vurugu kati ya makomandoo wa timu hizo
wamepambana kwa kuzichapa vibaya.
Makomandoo hao wamezichapa mara baada ya
wachezaji wa Simba kuingia uwanjani na kukatiza katikati ya uwanja huku ikiwa
ni dakika 5 baada ya basi lao kuingia uwanjani likiwa tupu.
Wakati basi linaingia uwanjani,
mashabiki wa Mbeya City waliojazana kwa wingi uwanjani hapo walilizomea
wakidhani lina wachezaji hao, lakini kumbe lilikuwa tupu.
Dakika tano baadaye huku maswali yakiwa
yamejaa uwanjani hapo, wachezaji wa Simba walianza kuingia wakitembea taratibu
na kukatiza katikati ya uwanjani hali iliyosababisha kuzuka kwa tafrani hilo na
mwisho, polisi wakaingilia na kuamua ugomvi na wachezaji wa Simba waliokuwa
wakishuhudia ugomvi huo kama muvi, wakaingia vyumbani.







0 COMMENTS:
Post a Comment