Pamoja na kufungwa mabao 2-0 na
Ferreviario ya Msumbuji na kutolewa kwa jumla ya mabao 2-1, wachezaji wa Azam
FC leo wamerejea jijini Dar wakiwa na furaha tele.
Wachezaji hao, hasa wale wa kigeni
walionekana na furaha ambayo haikupishana na ile ya Yanga ambao walifanikiwa
kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa
Komoronize kwao Moroni kwa mabao 5-2 na kukamilisha idadi ya mabao 12-2.
Hata kama wangekuwa na furaha, bado
wachezaji wa Azam FC walipaswa kuonyesha maumivu yao na hasa kwa kuwa wakati
wanashiriki mara ya tatu michuano hiyo, safari ya tatu ndiyo wametolewa mapema
zaidi.
Angalau kidogo baadhi ya wachezaji hasa wale wazalendo walionyesha kutokuwa na nyuso za furaha, hali inayoweza kuonyesha hawakufurahishwa na kuishia hapo.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment