Kocha wa zamani wa Azam FC, Stewart Hall
leo alimsimamisha kiungo wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’ na kupiga naye stori
kiana.
Hall alizungumza na Chuji ambaye ndiyo
alikuwa amewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
akitokea Comoro pamoja na wachezaji wengine wa Yanga.
Hall aliwasalimia asilimia kubwa ya
wachezaji wa Yanga, lakini baada ya hapo akaendelea kupiga stori na Chuji.
Baada ya mazungumzo mafupi, Hall
alimuachia Chuji ajiunge na wenzake ambao walikuwa wametangulia kwenye basi la
Yanga lililokuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kuwapokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment