Mechi ya pili ya raundi ya kwanza
kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na
Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga Stars tayari imeingia kambini
kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars
chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume
ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.
Shepolopolo iliibuka na ushindi wa
mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa
kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe.
Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.
Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini
ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther
Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma
Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja,
Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida
Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
0 COMMENTS:
Post a Comment