Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
liko katika hatua ya mwisho kumtangaza kocha mpya na inaelezwa atakuwa ni raia
wa kati ya nchini mbili, Ujerumani au Uholanzi.
Tayari TFF imemtupia virago Kocha Kim
Poulsen ingawa imekuwa ikielezwa kuwa imefanya hivyo kwa kukubaliana naye kamba
wavunje mkataba.
TFF chini ya Malinzi ilionekana
kutoridishwa na kasi ya Poulsen tokea ilipoingia madarakani.
Fununu za yeye kupoteza kazi zikaenea
lakini bado maofisa wa TFF wakawa ‘wanafunika kombe’ kiana.
Lakini leo, rasmi TFF imetangaza
kumalizana na Mdenishi huyo ambaye alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Mdenishi
mwingine, Jan Poulsen.
0 COMMENTS:
Post a Comment