Winga mwenye kasi wa Ashanti United, Said Maulid ‘SMG’, amekumbwa na tatizo jipya la kuugua kila
inapokaribia mechi ya Ligi Kuu Bara.
Tangu
kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo, SMG hajacheza mechi yoyote ambapo
Ashanti imecheza mechi tatu.
Awali
alikuwa akisumbuliwa na goti lakini baadaye akapona akajiunga na wenzake kwa
ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili, siku chache kabla ya kuanza kwa ligi
akajitonesha na hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kadhaa zinapokaribia mechi.
Kocha
Mkuu wa Ashanti, Abdallah Kibadeni amesema SMG anakuwa mzima wakati wa mazoezi
lakini mechi zinapokaribia lazima ajitoneshe.
“Unaweza
kumuona mzima siku zote na anafanya mazoezi lakini zinapobaki siku chache kabla
ya mechi, anajitonesha au anaumia.
“Angekuwa
ni kijana mdogo ningesema anaogopa mechi lakini huyu SMG ni mtu mzima, naamini
hawezi kuniongopea, hii ni dalili ya mtu kuelewa anachokifanya, kama angekuwa
ana tamaa angetaka kucheza hivyohivyo,” alisema Kibadeni.
Kesho
Jumamosi, Ashanti itavaana na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi, Kibadeni
anasema kama SMG akiendelea kuwa fiti anaweza kumtumia kwenye mechi hiyo.








0 COMMENTS:
Post a Comment