Simba imetamba kwamba itatibua rekodi ya
Mbeya City kutofungwa hata mechi moja kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa
Sokoine.
Kikosi cha Simba ambacho kipo Mbeya,
kesho kina kazi ya kupambana na Mbeya City kwenye uwanja huo na katika mechi ya
mzunguko wa kwanza, zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa, City
wakisawazisha zote mbili.
Katika Ligi Kuu Bara, Mbeya City iliyo
katika nafasi ya tatu, imepoteza mechi moja tu na yenyewe ni ugenini dhidi ya
Yanga.
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola
amesema wamepania kushinda na wanajiandaa vilivyo kuhakikisha wanashinda mechi
hiyo.
“Tunaweza kuvunja hiyo rekodi, huu ni
mpira na hata kama wanajiamini na sisi tunajiamini na tunachotaka ni ushindi,”
alisema.
“Wachezaji wote wako safi na
tumejiandaa, tunachosubiri ni muda wa kuingia uwanjani na kufanya kazi yetu,”
aliongeza nahodha huyo wa zamani wa Simba.
Simba imekuwa ikisuasua, kwani katika
mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu Bara imetoka sare dhidi ya Mtibwa Sugar na
kuchapwa 1-0 na Mgambo.








0 COMMENTS:
Post a Comment