Kikosi cha Yanga kipo kamilini ugenini
Moroni nchini Comoro kuwamaliza wenyeji wao Komorozine.
Katika mechi hiyo ya marudiano ya Ligi
ya Mabingwa Afrika inayosubiriwa kwa hamu mjini humo, Yanga imesisitiza ipo
kamili.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema
amepewa taarifa kwamba kesho watafanya kila linalowezekana kuibuka na ushindi.
“Hata kama katika mechi ya kwanza
tulishinda kwa mabao saba bila, lakini bado tunahitaji ushindi na wachezaji
wanalijua hilo.
“Nimeambiwa kikosi kipo fiti na
tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunashinda,” alisema.
Yanga iliitwanga Komorozine bao 7-0
katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na sasa inahitaji sare
ya aina yoyote au hata ikipoteza 6-0 bado itasonga mbele.
Baada ya hapo, Yanga ikisonga mbele
itakutana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly na mechi itaanza kupigwa jijini Dar Machi
Mosi kabla ya kurudiana wiki moja baadaye.








0 COMMENTS:
Post a Comment