February 24, 2014


Zikiwa zimebaki mechi saba ili Ligi Kuu ya Tanzania Bara imalizike, mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe, ameshafikisha idadi ya mabao yaliyofungwa na Kipre Tchetche, msimu uliopita.


Kipre, msimu uliopita alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 17 kwenye ligi kuu, lakini mabao mawili ambayo Tambwe alifunga jana yameshamfanya afikie idadi hiyo.

Hii ni rekodi mpya inawekwa na mshambuliaji huyo raia wa Burundi ya kufikia idadi ya mfungaji bora wa msimu uliopita zikiwa zimebaki mechi nyingi.

Kipre msimu huu hayupo kwenye kiwango kizuri hali ambayo imekuwa ikimpa nafasi kubwa Tambwe ya kuwika kwenye mbio za ufungaji bora.

Nyuma ya Tambwe ambaye huu ndiyo msimu wake wa kwanza, yupo Kipre mwenye mabao 10 na Elias Maguli tisa, hali ambayo inaonyesha ni vigumu kumkuta kinara huyo.

Tambwe anashikilia rekodi nyingine ya kufunga mabao matatu hat trick mbili kwenye michezo miwili ya ligi hiyo msimu huu na inaonekana kuwa anaweza kufunga mabao mengi zaidi na kuweka rekodi nyingine kuanzia ligi imeanza kuchezwa na timu 14.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic