Siku moja tu baada ya kutoa kauli
kwamba hamjui wala kumhofia hata kidogo, Kipre Tchetche wa Azam FC,
mshambuliaji Amissi Tambwe wa Simba ameonyesha alisema anachokiamini.
Leo amefanikiwa kufunga mabao matatu
katika mechi dhidi ya Oljoro na kufikisha mabao 13.
Kipre alimfikia Tambwe kwa kufunga bao
la 10 baada ya kufunga bao pekee wakati Azam FC ilipoichapa Rhino 1-0, juzi.
Lakini Tambwe akaiambia SALEHJEMBE, “hamjui
wala hababaiki” na leo hilo limethihirika kwa kupiga hat trick.
0 COMMENTS:
Post a Comment