February 1, 2014


MPIRA UMEKWISHA
Dk 4 za nyongeza
Dk 4 kabla ya mpira kwisha, Tambwe anatoka kwenye benchi na kupata maelezo namna ya kupewa mpira wake



Dk 85, Uhuru tena akiwa amebaki na kipa anashindwa kufunga
Dk 81, Simba wanafanya shambulizi tena na Chanongo anaboronga akiwa na kipa, Loga anasimama na kumfokea
Dk 74 Uhuru anashindwa kufunga akiwa na kipa
Dk 67, Ivo anagongana na Aziz Yusuf wakati akijaribu kuokoa, anaumia, anatibiwa na kuendelea


Dk 64, Uhuru Selemani anaingia kuchukua nafasi ya Kiemba aliykuwa amevaa kitambaa cha unahodha, anakichukua na kwenda kumvisha Ivo Mapunda
Dk 61, Oljoro ndiyo wanaingia kwenye 18 ya Simba kwa nguvu, lakini hakuna lolote
Dk 58, Simba inamtoa Tambwe ambaye amefunga mabao matatu na nafasi yake inachukuliwa na Abdulhalim Humud


Dk 55, Messi anatoka anaingia Said Ndemla
GOOOOOOOOOOO Dk 52, HAT TRICK kwa Tambwe, anafunga bao safi baada ya kuunganisha krosi ya Chanongo.


Dk 49, Kocha Loga wa Simba anapiga teke chupa ya maji baada ya Chanongo kuzabaa na mpira na kupokonywa.
Dk 47, Mkina anakosa bao, anapiga shuti kuubwa akiwa kwenye nafasi nzuri
DK 46, Mashabiki Yanga wanamzomea Ivo wakitaka atoe taulo lake nyavuni
HALF TIME:
Simba wanawala zaidi kipi cha kwanza, olojoro wanacheza vizuri lakini ni mpira wenye pasi nyingi na hatari kidogo
GOOOOOO Dk 29, krosi safi ya Chanongo aliyetoka kwa kasi inamkuta Tambwe, hajafanya utani na kufunga bao la tatu.


Dk 27, Shija Mkina anasukumwa ndani ya eneo la 18, lakini mwamuzi anasema acha kuregea, inuka na upige kazi
GOOOOOO Dk 24, Tambwe anaifungia Simba bao la pili baada ya krosi safi ya Messi huku mabeki wa Oljoro wakijaribu kumzua na kumsahau mfungaji


Dk 21, Oljoro wanafanya shambulizi lakini mpira dhaifu wa Majaliwa Mbaga unadakwa na Ivo.
Dk 19, Shuti la Tambwe linapita juu kidogo ya lango
GOOOOOOO Dk 12, Jonas Mkude anaifungia Simba bonge la bao baada ya kupiga shuti nje ya 18.
Dk 2&4, Simba wanashambulia zaidi na kuwapa wakati mgumu zaidi wageni Oljoro.


KIKOSI SIMBA..
Ivo, William Lucian, Baba Ubaya, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadhi Juma, Amri Kiemba, Amissi Tambwe Singano 'Messi' .



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic