Wachezaji wawili
wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars inayojiandaa na mchezo wa marudiano
dhidi ya Zambia itakayopigwa leo Ijumaa, Chamazi, Dar wameenguliwa kwenye kikosi
hicho kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.
Wachezaji hao
ambaoni Mwapewa Mtumwana na Flora Kayanda waliondolewa kwenye kambi ya timu hiyo
iliyopo kwenye hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar tangu Jumapili
ya wiki iliyopita.
Chanzo makini
kutoka ndani ya timu hiyo kimesema, wachezaji hao walienguliwa
baada ya kubainika kuwa walitumia kilevi wakiwa bado wapo kambini.
“Waliondoka kwenda
kutembea Jumapili, waliporudi jioni walikuwa wamelewa na ilionekana walikunywa
pombe nyingi,” kilisema chanzo.
Alipotafutwa Nasra
Mohammed ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo alisema: “Kweli tumewaondoa kutokana
na matatizo mbalimbali ya utovu wa nidhamu lakini sitaweza kulizungumzia sana.”
0 COMMENTS:
Post a Comment