Timu ya Taifa ya Zambia (Shepolopolo)
inatua nchini kesho mchana (Februari 27 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya
marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Tanzania (Twiga
Stars) itakayochezwa keshokutwa (Februari 28 mwaka huu).
Shepolopolo yenye msafara wa watu 29
itawasili kwa ndege ya Fastjet ikitokea Lusaka na itafikia kwenye hoteli ya
Accomondia kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex ulioko
Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Waamuzi wa mechi hiyo kutoka Burundi
wakiongozwa na Ines Niyosaba wamewasili nchini leo asubuhi wakati Kamishna Fran
Hilton-Smith kutoka Afrika Kusini atawasili kesho (Februari 27 mwaka huu) saa 8
kamili mchana kwa ndege ya South African Airways.
0 COMMENTS:
Post a Comment