March 5, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
Bao alilofunga nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni gumzo kubwa katika jiji hili na hasa kwa kuwa hawajui lilifungwa namna gani.


Awali mashabiki wa jiji hili na kwingineko nchini Misri walikuwa na hamu ya kuuona mpira huo kama walivyoelezwa, lakini ikatokea hali ya kutoelewana kati ya Yanga na kampuni waliyoingia nayo mkataba ionyeshe, mechi haikuonyeshwa.

Kutokana na hali hiyo, mashabiki wamekuwa wakitaka kujua walifungwa vipi bao hilo na hasa wakisikia kuwa lilikuwa ni la kichwa imekuwa ikiwashangaza na wanaona si sahihi kufungwa bao la namna hiyo.

“Wanataka kujua sana lilikuwa bao la namna gani,” anasema mmoja wa Watanzania wanaoishi hapa. “Wana kawaida moja hapa, mashabiki wao hutaka kujua nani aliyefanya kosa au lilianzia wapi.”

“Hivyo wanapenda kujua, tatizo lilitokea wapi. Ingawa kumekuwa na taarifa kwamba ni uzembe wa mabeki ndiyo walimruhusu Cannavaro kuwamaliza. Maana hata siku walipovamia pale klabuni walikuwa wakiimba na kuwalaumu mabeki kuwa wamewamaliza.”

SOURCE: CHAMPIONI NEWSPAPER

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic