March 5, 2014


Na Mwandishi Wetu, Cairo
Mashabiki wa mabingwa wa Afrika, Al Ahly wana hasira ile kinoma, wakati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anaimaliza timu yao jijini Dar, wao tayari walikuwa wakimalizia mipango ya kuvamia klabuni kwao jijini hapa.

Mashabiki hao watukutu, walivamia klabuni kwao na kuanza kufanya vurugu huku wakiimba na kupinga kutokana na kufungwa bao 1-0 katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Baada ya kuvamia, taarifa zinaeleza kwamba walitoka na kuingia mitaani hali iliyosababisha wapambane na askari polisi, hali hiyo imezua hofu, kwamba huenda ikakatazwa tena mashabiki kuhudhuria mechi hiyo.
Kumekuwa na hali fulani inayoonyesha kwamba mashabiki wa Al Ahly hawaamini kama timu kutoka ukanda w aAfrika Mashariki inaweza kukifunga kikosi chao, hivyo kupoteza mchezo huo ni uzembe mkubwa na wamekuwa wakiwatupia lawama mabeki.


Inaonekana wanaisubiri mechi dhidi ya Yanga kwa hamu kubwa na wanachotaka wamekuwa wakishinikiza kwamba lazima Ahly ishinde na isipofanya hivyo basi hawatakaa kimya hata kidogo, lazima watawaonyesha kazi waliofanya uzembe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic