Na Saleh
Ally, Cairo
Mabingwa wa
Afrika, Al Ahly ya hapa, wameamua kuondoka kwenye uwanja ambao wamekuwa
wakifanyia mazoezi na kujichimbia kusikojulikana.
Al Ahly
wameamua kufanya hivyo ili kufanya maandalizi yao kwa utulivu kabla ya kuivaa
Yanga katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumapili.
Katika
mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam mabingwa hao wa Afrika walilala kwa bao
1-0 lililofungwa na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kwa mara ya
kwanza Yanga ikafuta uteja wa kufungwa kila inapokutana na Al Ahly.
Lakini
mashabiki wao wengine wameeleza kuwa Ahly wameamua kujichimbia kutokana na
vurugu zilizofanywa na mashabiki wake mara baada ya kupata taarifa kuwa
wamefungwa bao 1-0 jijini Dar es Salaam.
“Wakati
mwingine imekuwa kawaida Ahl kuondoka na kujificha sehemu kwa ajili ya
maandalizi, lakini safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo, wanaonyesha
wmepania kushinda mechi hii.
“Tokea
wamerudi hawajaonekena klabu, huenda ni hofu ya mashabiki waliokuja kufanya
vurugu hapa wakipinga wao kufungwa na timu kutoka Afrika Mashariki, lakini pia
suala la umakini tu,” alisema mmoja wa wafanyakazi kwenye uwanja huo kwa
Kingereza cha tabu.
Championi
lilifunga safari hadi kwenye uwanja huo jana mapema kutaka kushuhudia mazoezi
yao, lakini likaambulia patupu na kuelezwa hivi: “Hutamuona mtu hadi siku ya
mechi.”
SOURCE: CHAMPIONI NEWPAPER
SOURCE: CHAMPIONI NEWPAPER
0 COMMENTS:
Post a Comment