DALALI (KUSHOTO) AKIWA NA ISMAIL ADEN RAGE NA GEOFREY NYANGE 'KABURU' |
Aliyekuwa kuwa Mwenyekiti wa
Simba, Hassan Dalali, ameibuka na kusema kuwa bado anajifikiria juu ya kuamua
kugombea au kutogombea nafasi hiyo kwa kuwa mwenyekiti wa sasa, Ismail Aden
Rage, anamaliza muda wake na ameshatangaza kutogombea tena.
Simba inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Mei nne, mwaka huu baada
ya muda wa uongozi wa Rage kumalizika huku akitangaza kutogombea tena nafasi
hiyo.
Dalali alifunguka kuwa kwa sasa bado hajafanya maamuzi sahihi ya kujua
kama atagombea au hatagombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
hivi karibuni.
“Mimi nimekuwa nikisikia tu kupitia vyombo vya habari kuwa, natarajia
kugombea lakini ukweli ni kwamba bado sijafanya maamuzi yoyote hadi sasa kujua
kama nitagombea au la.
“Muda ukifika nitaweka wazi kila kitu kwa kuwaita waandishi na kuweka
wazi kila kitu lakini kwa sasa sijaamua,” alisema Dalali.
0 COMMENTS:
Post a Comment