Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) na Benki ya CRDB zimeunda kikosi kazi (task
force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi za elektroniki ambayo
yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza.
TFF na
CRDB zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya
tiketi za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya
uboreshaji matumizi ya mfumo huo.
Kikosi
kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe
wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na
Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.
Rais wa TFF,
Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya
CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao akiongoza timu
yake.
Malinzi
amesema ni imani ya TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa
ulinzi wa mapato milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha
matumizi hayo ya tiketi za elektroniki.
0 COMMENTS:
Post a Comment