Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC, Kelvin Friday, amesimulia jinsi alivyofanikiwa
kumfunga kipa wa Yanga, Juma Kaseja, kwa shuti kali na kusema alitamani siku
moja afanye tukio kama hilo.
Azam ilipata sare katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa
Taifa, juzi ambapo bao hilo lilikuwa la kusawazisha na hivyo kuendeleza rekodi
ya kutopoteza mchezo kwenye ligi hiyo msimu huu.
Friday amesema amejisikia furaha kufanikiwa kumfunga Kaseja na
kuifungia timu yake bao zuri japo haikuwa kazi rahisi kwao kurudisha bao lile
kutokana na ugumu wa mchezo.
“Nimefurahi sana kufanikiwa kumtungua Kaseja, si jambo dogo kabisa
kutokana na upinzani uliokuwemo katika mchezo ule, nilitamani sana siku moja
kumfunga Kaseja.
“Baada ya furaha hiyo, sasa tunaangalia mbele jinsi ya kujipanga kwa
michezo mingine na kuendelea kutetea rekodi yetu ya kutopoteza mchezo,” alisema
Kelvin.
0 COMMENTS:
Post a Comment