March 5, 2014

JIJI LA CAIRO LINAVYOONEKANA USIKU
Na Saleh Ally, Cairo
Hali ya hewa ya jiji la Cairo, Misri leo imebadilika ghafla na kufikia nyuzijoto 31 ambazo ni sawa na Dar es Salaam.

Hali hiyo ya hewa ilibadilika leo mchana na kusababisha watu kuanza kulalamika kuwa ni joto kali.
Kwa siku zote tatu, hali ya hewa imekuwa ni kuanzia nyuzijoto 18 hadi 23.
Hali ya hewa ikiwa hivyo, itazidi kuipa Yanga nafasi ya kuwa katika hali nzuri zaidi, kwa kuwa itakuwa iko sawa na nyumbani.
Awali kulikuwa na hofu ya kuikuta Cairo ikiwa na baridi kali ambayo ingeisumbua Yanga.
Hata hivyo, jioni hii hali hiyo ya baridi imeongezeka kidogo angalau kufikia nyuzijoto 26.

Lakini kwa hali ilivyo, Yanga inayotua kesho alfajiri haiwezi kuwa katika wakati mgumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic