March 5, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
Hali ya joto imeongezeka kwa kiasi fulani, kutoka nyuzi 18 hadi 20 kwa leo.
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wanawasili kesho hapa kuwavaa mabingwa wa Afrika, Al Ahly.

Mechi hiyo itapigwa Jumapili jijini hapa na hali ya joto huenda ikawa nzuri zaidi kwa Yanga.
Lakini inaonekana Al Ahly walikuwa wakitaka kuwe na joto zaidi ili kuwapa Yanga wakati mgumu.
Bado inaonekana dalili za kushuka kwa nyuzijoto kutakuwa nadra na huenda mwisho ikawa 18 ambayo haitawapa Yanga wakati mgumu.
Kijua kimetoka, hali inayoashiria kuwa Yanga hawatakuwa na tatizo la hali ya hewa ambalo ni bora kwa kikosi hicho kutoka Tanzania.

Awali kulikuwa na hali ya hofu kwamba huenda baridi kali ya Cairo ingeipa Yanga wakati mgumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic