March 5, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
Bado kuna matumaini makubwa kwa mashabiki wa soka jijini hapa kwamba, lazima Al Ahly itaing’oa Yanga.


Mashabiki hao wanaamini kuwa bao 1-0 waliloshinda Yanga, haliwezi kuisumbua timu hiyo.
Katika mahojiano na mashabiki tofauti katikati ya jiji hili, mashabiki wengi wameonyesha kuwa na imani na Ahly.
“Kweli Yanga wameshinda kwao, hapa waafungwa. Lazima Ahly watasonga mbele, hawawezi kukubali kufanya utani,” alisema mmoja wa shabiki wa Ahly.
Shabiki mwingine alisema Ahly wako katika tahadhari kubwa, kwa kuwa suala la kufungwa limewakera mashabiki.
“Wanajua hatujapenda, lakini mara nyingi tuna subira. Nafasi hiyo hawawezi kuifanyia utani.”

Yanga na Ahly zinavaana Jumapili jijini hapa ingawa bado suala la mashabiki ni kizungumkuti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic