Kampuni ya mawasiliano ya Airtel
Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Mimi ni Bingwa’ imemfanya Bw. Rashid Jacob
Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kuwa tajiri baada ya kujishindia
milioni 50 katika droo kubwa ya bahati nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Akimtangaza mshindi Meneja Uhusiano
wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Leo hii tumefikia mwisho wa
promosheni yetu ya ‘Mimi ni Bingwa’ ambayo imewanufaisha watanzania walio
wengi. Limekuwa ni zoezi lenye mafanikio makubwa likiwa na idadi kubwa ya
wateja wakijiunga katika promosheni na kujishindia zawadi katika vipengere
tofauti.
“Ningependa kuwashukuru wateja wetu
kwa kushiriki katika promosheni hii tangu ilipoanza mwishoni mwa mwezi November
mwaka jana. Airtel bado mipango mingine mingi inakuja, tukilenga kuendelea
kurudisha kile tulichonacho kwa wateja wetu na kuisaidia jamii inayotuzunguka
kukuza viwango vyao vya kuishi,” alisema Mmbando.
Alisisitiza kuwa mbali na zawadi
kubwa ya milioni 50 kutolewa, washindi wa awamu ya pili na ya tatu wa safari
iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya moja kwa moja ‘live’ ya
klabu ya Manchester United wataondoka nchini mwezi huu pale klabu hiyo
ikitarajia kucheza tena katika uwanja wa Old Trafford.
Kwa upande wake, milionea mpya
akizungumza kupitia simu kutoka Bukoba aliipongeza Airtel Tanzania kwa
kuanzisha promosheni zinazosaidia kuyabadilisha maisha ya wateja wake na kuleta
mabadiliko chanya katika jamii na nchi nzima kwa ujumla.
“Hii ni miujiza inayotokea maishani
mwangu. Siwezi kuamini nami nimeingia katika orodha ya mamilionea Tanzania. Ni
kama ndoto kwangu imekuwa kweli sababu ya Airtel. Naishukuru Airtel Tanzania
kwa msaada wao si tu kwa wateja wake bali pia kwa jamii yote inayoizunguka.
Hizi milioni 50 hakika zitabadilisha maisha yangu kabisa na zawadi
nitakayoipatia Airtel ni kubaki kuwa mteja wao mwaminifu wakati wote,” alisema
Bw. Kagombola.
“Nimejiunga na promosheni ya Airtel
‘Mimi ni Bingwa’ tangu ilipoanza mwezi November, na nilikuwa nikicheza pale tu
nitakapokuwa na salio la kutosha. Ilikuwa ni changamoto kuweza kupata pesa ili
kuongeza salio la muda wa maongezi, lakini siwezi kuamini leo hii mimi ni
milionea! Shukrani ziende kwa promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kubadilisha
maisha yangu,” aliongeza.
Promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’
imeanza mwezi Novemba mwaka jana, ikiwa ni matokea ya ushirikiano katika ya
klabu ya Manchester United na kampuni hiyo ya simu, haikulenga kuwazawadia
wateja pekee, bali pia kuwaunganisha washiriki na soka la kimataifa na kusaidia
kukuza hari ya michezo miongoni mwa watanzania.
Wakati wa promosheni hiyo, washiriki
wawili wa Mimi ni Bingwa walizawadiwa shilingi milioni 2 kila siku, wawili
wakijishindia shilingi milioni 5 katika droo za kila wiki na mmoja kujishindia
tiketi mbili za safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.
0 COMMENTS:
Post a Comment