March 5, 2014


Na Saleh Ally, Cairo
Hali imezidi kuwa tata kuhusiana na suala la mashabiki waingie au la.

Hadi jioni ya leo, jibu la ndiyo au hapana halikuwa na uhakika na
Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Alexandria, Said Nasser ameviambia vyombo vya habari leo kwamba bado hawajapata ufumbuzi wa suala hilo.
“Hata ndani ya saa nne zijazo itakuwa bado, hivyo tunaomba mtupe muda.
“Tuna nafasi ya kuzungumza kesho na kupata ufumbuzi wa uhakika kuhusiana na suala hilo,” alisema.
Dalili zinaonyesha huenda kusiwe na watazamaji katika mechi hiyo ya Jumapili kati ya Yanga dhidi ya Ahly jijini hapa.
Hali hiyo inatokana na vurugu za mashabiki ambao tayari wameonyesha hali ya kulazimisha timu yao ishinde.

Iwapo itapoteza mchezo au kushindwa kusonga na wao wakiwa uwanjani, basi lazima zitazuka vurugu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic