Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa)
kimefanya uchaguzi wake jana kwenye Ukumbi wa Water Fronti na kupata viongozi
wapya.
Akizungumza kabla ya kutangaza matokeo hayo Katibu
Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi wa Taswa Mwina Kaduguda alisema anawapongeza
waandishi wa habari kwa kutimiza wajibu wao kwa kuchagua viongozi hao.
“Niwapongeze wote ambao mpaka sasa mpo humu
ndani, najua katika uchaguzi wowote lazima kutatokea matatizo ya hapa na pale,
lakini wajumbe mmetumia demokrasia yenu,” alisema.
Pia Kaduguda alitoa somo kwa viongozi ambao
wameshinda kuhakikisha wanatimiza na kuyafanya yale ambayo waliwahaidi wapiga
kura kabla ya kuwachagua.
Kaduguda ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu klabu
ya Simba aliwataja kwa upande walioshinda nafasi ya wajumbe wa Taswa Hassan
Bumbuli, Ibrahim Bakari, Mroki Mroki, Musa Juma, Chacha Maginga, Rehule
Nyaulawa na Mwani Nyagasa.
Nafasi ya Mhazini Msaidizi ilichukuliwa na Zena
Chande aliyemsindia mpinzani wake Elius Kambili, huku Mhazini Mkuu ikichukuliwa
na Shija Richard aliyemshinda Mohamed Mkangara.
Kwa upande wa Katibu Msaidizi aliyeshinda ni
Grace Hoka, huku nafasi ya Katibu Mkuu ikichukuliwa na Amiri Mhando ambaye
alikuwa akitetea nafasi hiyo na alipigiwa kura za ndio na hapana kutokana na kugombea nafasi hiyo peke yake na
kushinda kwa kishindo.
Kwa upande wa Mwenyekiti Juma Pinto amerejea
tena madarakani kwa kupigiwa kura za ndio na hapana baada ya nafasi hiyo
mgombea akiwa pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment