Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji,
inaonyesha mapema alijua wanaibwaga Al Ahly.
Maana alijitokeza mapema na kuwaamsha mashabiki
kwamba washangilie kwa nguvu vijana wao wataingia kazini.
Manji alifanya hivyo huku akionyesha
kujiamini kupita kiasi, kabla ya kurudi ndani na baadaye akaonekana akiwa jukwaani.
Yanga ilimaliza dakika 90 kwa kuimaliza
Al Ahly kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment