Kocha Mkuu wa
Yanga, Hans van Der Pluijm, juzi alipandwa na hasira nusura amchape
makonde beki wake, Kelvin
Yondani.
Yanga ilivaana na Mgambo JKT kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga na kula kichapo
cha mabao 2-1.
Tukio hilo lilitokea mara baada ya mchezo kumalizika ambapo Pluijm alimfuata Yondani aliyekuwa
amesimama na kuanza kumlalamikia kwa madai kuwa beki huyo alifanya kosa
kusababisha penalti iliyozaa bao la pili kwa Yanga.
Wakati kocha huyo alionekana kukasirika huku akiongea kwa
ukali, Yondani alionyesha hali ya kutojali na kutaka kuondoka kwenda kwenye
gari lakini Pluijm alimvuta mkono kwa nguvu na kuendelea kumpa dozi ya maneno.
Hata hivyo, waandishi waliokuwa wanamsubiri kocha huyo ili
awape tathimini ya mchezo ndiyo waliomuokoa Yondani baada ya kumvuta mwalimu
huyo ili wafanye naye mahojiano na Yondani ambaye hakujibu kitu na kuingia moja
kwa moja kwenye basi la wachezaji wa timu hiyo lililokuwa karibu naye.
“Lile tukio la pale uwanjani si uliliona jinsi kocha
alivyokuwa akimfokea Yondani? Hali haikuishia hapo, kocha alipanda tena kwenye
basi na kwenda mpaka alipokaa Yondani na kuendelea kumpa dozi.
“Kweli kocha alikuwa amekasirika sana, nafikiri Yondani
alifanya vizuri kutomjibu kama angemjibu labda angempiga hata makofi,” kilisema
chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment