April 2, 2014

 Chelsea imeanza vibaya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji wake PSG.
Katika mechi iliyopigwa punde wenyeji walianza kupata bao katika dakika ya Lavezzi katika dakika ya 4, lakini Chelsea wakasawazisha katika dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalty kupitia Eden Hazard baada ya Oscar kuangushwa.

Kipindi cha pili, PSG walifunga mabao mawili wakianza na dakika ya 61 baada ya beki David Luiz kujifunga kutokana na mpira wa krosi kabla ya Javier Pastore kuwachambua mabeki wa Chelsea na kuandika bao la tatu katika dakika ya 90.
Mategemeo ya Chelsea ni katika mechi ya pili ambayo itapigwa mjini London na ili isonge inatakiwa kushinda kuanzia mabao 2-0.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic