April 2, 2014


Madrid imeanza vizuri hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Borussia Dortimund kwa mabao 3-0.


Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, wenyeji walipata bao la kwanza mapema kabisa katika dakika ya 3 kupitia Gareth Bale ambaye alifanya kazi ya ziada kuuwahi mpira aliopewa na kufunga.

Dakika ya 27, bwana mdogo fundi, Isco akatupia bao la pili na  mabao hayo mawili yakadumu hadi mapumziko.

Cristiano Ronaldo ndiye alifunga bao pekee katika kipindi cha pili baada ya kupokea pasi ya Luka Modric katika dakika ya 57.

Madrid ambayo ina kumbukumbu ya kutolewa na Dortmund katika Ligi ya Mabingwa msimu uliipita, inahitaji sare ya aina yoyote katika mechi ya marudiano ili kusonga nusu fainali.









0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic