Kiungo wa Coastal Union, Haruna Moshi
‘Boban’, amesema viongozi wa soka hapa nchini wanatakiwa kubadilika endapo
wanataka kuona soka la Tanzania linakua, vinginevyo haliwezi kuendelea.
Boban, kwa sasa pamoja na wachezaji
wenzake kadhaa, wamesimamishwa na uongozi wa Coastal ambao pia umeamua kwenda
kuwashtaki kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na utovu wa nidhamu
uliokithiri.
Kiungo
huyo amesema ili soka la hapa nchini liweze kukua, viongozi wa timu za ligi kuu
wanatakiwa kubadilika kwa kiasi kikubwa.
Boban alisema hayo hivi karibuni baada
ya kusikia uongozi wa timu yao umekwenda kuwashtaki TFF.
“Viongozi wetu katika timu za hapa
nchini wanatakiwa kubadilika kwa kiasi kikubwa ili kuweza kuhakikisha soka
linakua na hata wachezaji wenyewe wataupenda mpira kwa dhati kutokana na wale
wanaowaongoza.
“Hata sisi wachezaji tunaposema kuhusu
jambo fulani msitulaumu sisi tu, hata viongozi wetu muwaangalie wao, siyo kila
wanalolisema ni sahihi.
“Wanatakiwa kubadilika na hamjui labda
kwenye timu tunaishi vipi mpaka tunafikia hapa tulipo sasa,” alisema Boban
ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba aliyewahi kucheza soka la kulipwa nchini
Sweden.
0 COMMENTS:
Post a Comment