BURHANI (KULIA) AKIITUMIKIA TIMU YAKE DHIDI YA SIMBA |
Kipa namba moja wa Mbeya City, David
Burhan, yupo kwenye mchakato wa kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi
baada ya kupokea ofa mbalimbali kutoka nchi tatu tofauti.
Burhan ambaye aliisaidia timu yake
kupanda ligi kuu msimu huu, amefanikiwa kuonyesha uwezo mkubwa licha ya ugeni
kwani katika michezo 23 aliyocheza, ameruhusu mabao 15 pekee.
Burhan ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye kikosi cha City, amesema
mchakato huo unafanywa na wakala wake, Nassor Mussa ambaye ni Askari wa Kitengo
cha Upelelezi Iringa na kwamba tayari ameshapata ofa kutoka nchi za Kenya,
Zambia na Qatar.
Alisema pia kuna timu za hapa nchini
ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka msimu ujao na kwamba kwanza anawapa nafasi ya
kwanza Mbeya City kufanya nao mazungumzo na akiridhika na dau anaweza kubaki.
“Nashukuru Mungu mpaka sasa nimepokea
ofa nyingi sana kutona ndani na nje, wakala wangu ndiyo anafuatilia kila kitu
lakini tambua bado nina mkataba na Mbeya kwa hiyo nitawasikiliza wao kwanza
kabla ya wengine lakini zaidi ndoto zangu ni kucheza soka la kulipwa,” alisema
Burhan.
0 COMMENTS:
Post a Comment