Kocha Mkuu
wa Ashanti United, Abdallah Kibadeni, amesema Azam FC ilistahili kutwaa ubingwa
wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ina uwezo wa kila kitu lakini wachezaji wao ni wa
kawaida sana.
Azam
ilitawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu msimu wa 2013/2014 baada ya kuifunga Mbeya
City mabao 2-1 na kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Kibadeni alisema Azam ina wachezaji wa kawaida lakini ni
vyema kama wameshajua wamechukua ubingwa wakaanza kufanya usajili wa maana kwa
ajili ya kujiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Alisema
ushindi wao waliokuwa wakiupata ni mwepesi.
“Azam
walistahili ubingwa kwa kuwa ukiangalia utaona wanaweza kujimudu kwa kila kitu,
tofauti na hizi timu nyingine binafsi, lakini wachezaji wao wana uwezo wa
kawaida sana, cha muhimu wafanye usajili mwingine mapema kwa ajili ya kujiandaa
na michuano ya kimataifa,” alisema Kibadeni.
Kibadeni ni mchezaji nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars na anaingia katika rekodi ya mmoja wa washambuliaji bora nchini, pamoja na makocha waliofikia mafanikio ikiwa ni pamoja na kuipeleka Simba fainali za Kombe la Caf mwaka 1993.
0 COMMENTS:
Post a Comment