MESSI |
Wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Simba, beki
Donald Musoti na kiungo mshambuliaji Ramadhani Singano ‘Messi’, wameanza
mazoezi ya pamoja na timu hiyo baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na
kusumbuliwa na majeraha.
Wachezaji hao hawakuonekana kwenye mchezo wao wa
Jumapili iliyopita dhidi ya Ashanti, hali iliyowatia hofu mashabiki wa Simba
kama watacheza kwenye mchezo ujao dhidi ya Yanga.
SALEHJEMBE iliwashuhudia wachezaji hao
wakifanya mazoezi ya pamoja kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar juzi na
lilipomuuliza kocha mkuu Zdravko Logarusic kuhusiana na hali za wachezaji hao,
alisema walikuwa wakisumbuliwa na maumivu ya misuli lakini kwa sasa wapo sawa
na watakuwepo kwenye mchezo wa Jumamosi.
Alisema ana furaha kuona wachezaji hao muhimu wanarudi
kikosini japo wamebakiwa na mchezo mmoja lakini una umuhimu mkubwa kwani
wanataka kuonyesha kuwa japo wapo nafasi ya nne lakini wana uwezo mkubwa zaidi
ya Yanga.
“Messi na Musoti walikuwa
na maumivu ya misuli lakini daktari amethibitisha kuwa kwa sasa wapo fiti na
nina uhakika watakuwepo katika mechi yetu na Yanga na mashabiki wasiwe na
wasiwasi,” alisema Logarusic
0 COMMENTS:
Post a Comment