Kocha Zdravko Logarusic amesema anaamini atabaki Simba kama wao
watakuwa tayari kufanya hivyo.
Lakini akasisitiza, iwapo ataondoka nchini keshokutwa Ijumaa, basi
anaweza kuendelea na kusaka maslahi mbele kwa mbele.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Loga alisema anaona ni vizuri kuwapa
nafasi Simba ambao ni waajiri wake.
“Nikiona hawana mpango, basi nitaangalia kazi kwingine. Unajua vizuri
kutoa nafasi kwa mwajiri wako kwanza.
“Halafu utaona anakuhitaji au la, ikiwa anakuhitaji, basi utajua. Kama
hakuhitaji pia utajua,” alisema Loga.
Loga anatarajia kuondoka nchini Ijumaa kurejea kwao Croatia ikiwa
ni baada ya msimu kumalizika.








0 COMMENTS:
Post a Comment