Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesisitiza kuwa bado anataka kuifunga Yanga katika mechi yao ya mwisho.
Kikosi chake kimepoteza mechi dhidi ya
Ashanti United kwa kufungwa bao 1-0, lakini Logarusic akasisitiza kuwa bado
anataka kuifunga Yanga.
Simba imepoteza mwelekeo na makali,
lakini itamaliza mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.
“Tukiifunga Yanga tutakuwa tumeweka
heshima, tutakuwa tumewafurahisha mashabiki wetu hata kidogo kwa kuwa tumekuwa
na msimu mbaya.
“Kikosi changu bado kina uwezo wa
kuifunga Yanga, hamasa inahitajika na ninaona kwa ajili ya mechi hii tunaweza
kupata hamasa,” alisema.
Kwa msimu wa pili mfululizo, Simba
imekuwa haina nafasi tena ya kutwaa ubingwa au kuiwakilisha Tanzania katika
michuano ya kimataifa chini ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
0 COMMENTS:
Post a Comment