Na Saleh
Ally
ATLETICO
Madrid ndiyo vinara wa Ligi Kuu ya Hispania La Liga, haijawahi kutokea kwa
kipindi cha zaidi ya misimu nane timu nyingine kuwa katikati au juu ya Real
Madrid na Barcelona.
Kila timu
imebakiza mechi tano kumaliza La Liga na Atletico wana pointi 82 kileleni mwa
msimamo wa ligi hiyo ikifuatiwa na magwiji Real Madrid wenye pointi 79 na
Barcelona wenye 78.
Pamoja na
kuaminika Real Madrid na Barcelona ni lazima ziwe mabingwa kutokana na historia
ya ligi hiyo, lakini inawezekana kabisa Atletico kuwa mabingwa wa La Liga msimu
huu. Sababu ziko nyingi.
Pia
imezitambia Madrid na Barcelona kila walipokutana. Kuwa kileleni kwa Atletico
si la kubahatisha kwa kuwa timu hiyo kutoka jijini Madrid imefika hapo kwa
ubora ambao unaonekana wazi.
Takwimu:
Kitakwimu
Atletico imeshinda mechi 26 ambazo ni nyingi zaidi kuliko Real Madrid na
Barcelona ambazo kila moja imeshinda 25.
Atletico
Madrid imepoteza mechi tatu ambazo ni chache zaidi kuliko zile walizopoteza
Madrid ambazo ni nne na Barcelona tano.
Mechi nane:
Ukiangalia
mechi nane za mwisho za La Liga kwa kila timu kati ya hizo tatu, Atletico
Madrid bado inaonekana kuwa bora kuliko wakongwe hao wa Hispania.
Katika
mechi nane za mwisho, Atletico imeshinda saba na sare moja tu ambayo ndiyo
rekodi nzuri na ya juu katika kipindi hiki kwenye La Liga. Ubora wao umepanda
kwa asilimia 31.
Madrid wao
katika mechi hizo nane za mwisho, wameshinda tano, wamepoteza mbili na sare
moja na ubora wao umeshuka kwa asilimia 28.
Kwa upande
wa Barcelona katika mechi nane za mwisho, wameshinda sita na kupoteza mbili
ambayo pia si rekodi nzuri na imewaporomosha kwa asilimia 26 ya ubora wao.
Kwa takwimu
hizo, inaonekana wazi kuwa Atetico Madrid hawabahatishi tena na wanaweza
kufanya makubwa na kushinda La Liga, hasa kama watakuwa makini katika mechi zao
tano za mwisho.
Ligi ya
Mabingwa:
Utaona,
kawaida timu za Hispania ambazo huingia hatua ya nusu fainali ni Real Madrid na
Barcelona, lakini safari hii Atletico Madrid imeingia katikati na kuwaondoa
vijana hao kutoka Catalunia.
Hii ni
sehemu ya kuonyesha ni timu bora ya Hispania kwa kipindi hiki hasa kama
itaendelea kucheza kwa kiwango sahihi bila ya kuyumba.
Atletico
Madrid itacheza na Chelsea kutoka England, lolote linawezekana kwa kuwa Kocha
Diego Simeone si mgeni kwa Jose Mourinho wakati akiwa Real Madrid.
Hata kama
Mourinho atakuwa amehamia timu nyingine, bado ana nafasi ya kujua kipi afanye
ili kupambana naye.
Kikosi
hicho cha Simeone kimebakiza mechi tatu tu kuweka rekodi mpya ya kuwa Mabingwa
Ulaya na kwa ubora wao ni kitu kinachowezekana kabisa.
Iwapo
watafanikiwa kuchanga karata zao vizuri dhidi ya Chelsea, basi mechi ya mwisho
itakuwa ni fainali dhidi ya jirani zao Real Madrid au mabingwa watetezi Bayern
Munich.
Atletico
Madrid si yenye majina makubwa, mkali wao Diego Costa, pia Koke lakini bado
kuna wachapakazi kibao ambao hawana mbwembwe wala umaarufu na ndiyo silaha ya
vijana hao wa Simeone.
LA LIGA
IMESHINDA IMEPOTEZA
SARE POINTI
26 3 4 82
0 COMMENTS:
Post a Comment