Vyama
vya mpira wa miguu vya mikoa kumi vimewasilisha majina ya mabingwa wao
watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).
Mabingwa
hao ni Arusha (AFC), Kilimanjaro (Panone FC), Lindi (Kariakoo SC), Manyara
(Tanzanite SC), Mara (JKT Rwamukoma), Morogoro (Volcano FC), Mtwara (Pachoto
Shooting Stars), Pwani (Kiluvya United), Shinyanga (Bulyanhulu FC), Singida
(Singida United) na Tanga (African Sports).
Mikoa
ambayo haijawasilisha mabingwa wake ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa,
Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Simiyu na Tabora wakati mikoa ya Dodoma na Mwanza imeomba
kuongezewa muda kutokana na sababu mbalimbali.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) iliagiza kuwa mikoa yote iwe imemaliza ligi na kuwasilisha jina la bingwa
wake Machi 30 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment