SIMKOKO |
Kikosi
cha watu 27 wakiwemo wachezaji na benchi la ufundi cha timu ya Taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kinatarajia kuondoka
keshokutwa (Aprili 3 mwaka huu) kwenda Nairobi, Kenya.
Ngorongoro
Heroes inayofundishwa na John Simkoko ipo kambini tangu Machi 23 mwaka huu
kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya (U20). Mechi hiyo ya michuano ya Afrika kwa
vijana wenye umri huo itachezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka huu) saa 10 kamili
jioni Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (Aprili 1 mwaka huu), Kocha Simkoko
amesema wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mechi hiyo, na nia ni kupata
matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini wiki tatu
baadaye.
Kikosi
cha Ngorongoro Heroes chenye wachezaji 20 na viongozi saba kitaondoka saa 4.30
asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Msafara wa timu hiyo utaongozwa na mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ayoub
Nyenzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana.
Mechi
hiyo itachezeshwa na waamuzi Abdoulkarim Twagiramukiza, Ambroise Hakizimana,
Raymond Bwiliza na Louis Hakizimana wote kutoka Rwanda wakati Kamishna ni
Maxwell Mtonga wa Malawi.
Ngorongoro
Heroes itaagwa kesho (Aprili 2 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment