April 1, 2014





Ndugu na rafiki, jana walivamia nyumbani kwa mshambuliaji Mrisho Ngassa wa Yanga na kumfanyia bonge la sapraiz.

Watu hao ambao walifika nyumbani bila ya Ngassa kujua walikuwa wanataka kufanya nini waliingia wakiwa na keki na mara moja wakaanza kuimba kumpongeza siku yake ya kuzaliwa.

Ngassa alikuwa hajajua lolote kwa kuwa alikuwa amesahau kuhusiana siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akiugulia maumivu ya kushindwa na Mgambo Shooting mjini Tanga.

“Sikuwa na ujanja, niliungana nao na tukasherekea pamoja na ninawashukuru sana kwa kuonyesha upendo kwangu,” alisema Ngassa aliyechipukia kisoka mkoani Mwanza.
Ngassa amerejea Yanga kwa mara ya pili akitokea Simba ambayo aliichezea baada ya kupelekwa kwa mkono na Azam FC ambayo pia ilimnunua kutoka Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic